Barcelona Macho yote kwa Nico Williams

Klabu ya Barcelona macho yao yote yapo kwa winga wa Athletic Club raia wa kimataifa wa Hispania Nico Williams kuelekea msimu ujao wa mwaka 2024/25.

Barcelona inaelezwa usajili ambao wanautolea sana macho ni Nico Williams kuhakikisha wanapata saini yake kutokana na ubora ambao yuko nao mchezaji huyo, Klabu hiyo inataka kuhakikisha msimu ujao wanakua na mawinga bora sana ndani ya klabu hiyo kwakua kwasasa wana Lamine Yamal.barcelonaBarca wanataka kuhamishia ushirikiano wa Yamine Yamal na Nico Williams ambao wanauonesha ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania na kuupata ndani ya klabu yao, Wachezaji hao wawili wamekua na ubora mkubwa sana ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania msimu huu.

Klabu ya Barcelona inaelezwa ilitaka kupeleka ofa kwa klabu ya Everton kwajili ya kumpata kiungo wao Amadou Onana ambaye tayari ameshakubali kujiunga na Aston Villa kwakua wanataka kuwekeza kiwango chao cha pesa kwajili ya kupata saini ya winga Nico Williams.

Acha ujumbe