AWESU AWESU NA SIMBA NI KAMA PICHA LA KIZUNGU

NYOTA Awesu Awesu rasta aliyetambulishwa kuwa kwenye changamoto mpya msimu wa 2024/25 ndani ya kikosi cha Simba kinachoolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Alitambulishwa kuwa mali ya Simba Julai 17 akitokea KMC, alijiunga na timu kambini Misri Julai 17 alicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki Simba Day,Agosti 3 na ametambulishwa kwa mara nyingine kurejea KMC,Agosti 13.AWESU AWESUInaelezwa kwamba KMC walipeleka kesi ya mchezaji huyo Shirikisho la Soka Tanzania kwa kulalamika kuwa Simba hawakufuata utaratibu kwenye suala la usajili wake hivyo Simba wameambiwa wanapaswa kufuata utaratibu.

Inatajwa kuwa Simba haikifuata utaratibu kwenye usajili wa Awesu Awesu ambaye alivunja mkataba wake wa mwaka mmoja a mabosi wake wa KMC.

Msimu wa 2023/24 Awesu alikuwa ndani ya KMC na uzi wake ulikuwa ni jezi namba 23 alikabidhiwa hiyo pia alipokuwa ndani ya kikosi cha Simba.

Kwenye mchezo wa Simba Day dhidi ya APR nyota huyo alipata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa wakati Simba ikishinda jumla ya mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Waajiri wake wa zamani wameandika namna hii kwenye ukurasa wa Instagram chapisho lilibeba picha yake: “Karibu tena nyumbani.”

Acha ujumbe