Arsenal Bado Wanampambania Merino

Klabu ya Arsenal inaendelea kupambania saini ya kiungo wa kimataifa wa Hispania Mikel Merino ambaye wanahitaji kupata saini yake kwajili ya kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao.

Arsenal wanafanya mazungumzo na klabu ya Real Sociedad kwa takribani wiki tatu sasa kwajili ya kupata saini ya kiungo wa klabu hiyo Mikel Merino, Hii ni kuhakikisha wanaiboresha timu yao kuelekea msimu wa 2024/25 ambapo wamepanga kufanya makubwa katika michuano ambayo watakua wanashiriki.arsenalKiungo Mikel Merino inaelezwa anataka kucheza kwa washika mitutu hao wa London hivo kwa kiwango kikubwa klabu hiyo chini ya kocha Mikel Arteta wanaamini kwa kiwango kikubwa wanaweza kupata saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye amefanya vizuri ndani ya klabu ya Real Sociedad.

Kiungo Mikel Merino kujiunga na klabu ya Arsenal ni suala la muda tu kwakua mchezaji huyo ameonesha kila nia ya kujiunga na miamba hiyo ya soka kutoka London Kaskazini, Hivo kinachoendelea kwasasa baina ya vilabu ni kuhakikisha wanapata muafaka mzuri ili mchezaji huyo ajiunge washika mitutu.

Acha ujumbe