Real Madrid Dhidi ya Atalanta leo Uefa Super Cup

Klabu ya Real Madrid leo itashuka dimbani kukipiga na klabu ya Atalanta katika mchezo wa Uefa Super Cup ambao unakutanisha bingwa wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya bingwa kombe la Europa league.

Real Madrid leo watacheza na Atalanta katika dimba la taifa wa la Poland linalopatikana katika jiji la Warsaw akitafutwa bingwa wa Uefa Super Cup, Mchezo maalumu kwajili ya kufungua rasmi msimu mpya wa michuano ya ulaya upande wa vilabu.real madridAtalanta chini ya kocha Gian Piero Gasperini ambao walitwaa taji la Europa league mbele ya Bayern Leverkusen ambayo haikua imefungwa mchezo hata mmoja, Leo watajaribu kuisimamisha Madrid kwenye mchezo  wa Uefa Super Cup kazi ambayo mara ya mwisho ilifanywa na Atletico Madrid 2018.

Kylian Mbappe leo atakua anacheza mchezo wake wa kwanza ndani ya Real Madrid baada ya kukamilisha usajili kutoka klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Hii ni fursa ya Mbappe kushinda taji lake la kwanza akiwa na mabingwa hao wa ulaya dhidi ya Atalanta ukitabiriwa kutokua mchezo mwepesi kutokana na ubora wa vijana wa kocha Gasperini.

Acha ujumbe