Real Madrid na Man United Vitani kwa Kinda wa Kifaransa

Klabu ya Real Madrid mabingwa wa ulaya imeingia vitani na klabu ya Manchester United katika kumuwania beki kijana mwenye kipaji kikubwa raia wa kimataifa wa Ufaransa Leny Yoro.

Leny Yoro (18) anayekipiga kwenye klabu ya Lille ameingia kwenye rada za klabu ya Real Madrid wakati huohuo Man United nao wanavizia saini yake, Jambo ambalo linafanya vilabu hivo viwili vikubwa kuingia vitani na kuangalia ni nani mwishoni ataibuka mshindi.Real MadridBeki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa amekua na msimu bora sana ndani ya kikosi cha Lille na kua moja ya wachezaji bora ndani ya kikosi hicho licha ya umri wake kua mdogo, Jmabo ambalo limefanya vilabu hivo kuvutana mashati kwajili ya saini yake.

Kijana huyo sifa zake kama mlinzi wa kati anayetumia mguu wa kulia ana uwezo wa kuzuia vizuri mipira ya chini na ya juu,Kimo pia anacho kizuri kama beki, Lakini pia ni mzuri kwenye kupiga pasi sahihi jambo ambalo linamfanya kua beki wa kisasa na kuu lulu sokoni kwakua sifa alizonazo ni sifa adhwimu kabisa sokoni.Real MadridLicha ya kua na ushindani mkubwa katika dili hili baina ya Real Madrid dhidi ya Man United kumuwania beki Leny Yoro, Vyanzo vya ndani kutoka nchini Ufaransa vinaeleza kua mabingwa wa ulaya wako kwenye nafasi nzuri ya kushinda vitaa hii kutokana na mchezaji mwenyewe kuipendelea klabu hiyo.

Acha ujumbe