Arsenal Yampoteza kinda Wake Matata

Klabu ya Arsenal imethibitisha kua kinda wake Chido Obi Martin (16) ataondoka klabuni hapo na kuelekea timu nyingine baada ya kushindwa kumshawishi kubakia kwenye timu hiyo.

Arsenal wanaelezwa walijitahidi kwa kiwango kikubwa kumpa ofa nzuri kinda Chido Obi Martin aendelee kusali ndani ya klabu hiyo, Lakini juhudi hizo hazikufua dafu kwani mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa kwani ameamua kwenda klabu nyingine kutafuta changamoto mpya.arsenalMchezaji Chido Obi Martin ambaye amekua kwenye kiwango bora sana kwenye timu ya vijana ya klabu ya Arsenal msimu uliomalizika jambo ambalo limefanya klabu hiyo kutaka kumpa mkataba mpya, Lakini mchezaji huyo kinda ameamua kutosalia ndani ya klabu hiyo licha ya ofa nzuri aliyopatiwa.

Klabu ya Manchester United inaelezwa ni moja ya timu ambazo zipo karibu kumsaini Chido Obi kwani Jumanne iliyopita mchezaji huyo aliitembelea klabu hiyo katika dimba la Old Trafford, Wakati ambao inasubiriwa kujulikana mchezjai huyo mwenye kipaji kikubwa ataelekea wapi Man United wanaelezwa wako karibu zaidi kumsaini Chido Obi Martin.

Acha ujumbe