Ayoub Lakred Apata Majeraha

Golikipa wa klabu ya Simba raia wa kimataifa wa Morocco Ayoub Lakred inaelezwa amepata majeraha akiwa kwenye kambi ya klabu hiyo iliyoko nchini Misri ambapo anaweza kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita.

Ayoub Lakred inaelezwa amepata majeraha ya misuli ya nyama za paja ambapo ndio yatamfanya akae nje ya uwanja kwa takribani wiki sita kwa maana ya mwezi mmoja na wiki mbili, Hivo kwa kipindi hichi klabu hiyo itakua na magolikipa wawili ambao ni Ali Salum  pamoja na Deo Abel.ayoub lakredGolikipa huyo wa kimataifa wa Morocco kukaa kwake nje ya uwanja kunaweza kuwapa changamoto klabu ya Simba kutokana magolikipa waliosalia wamekua hawana uzoefu wa kutosha, Wakati huo huo inaelezwa klabu ya Simba haipo kwenye mawasiliano mazuri na Aishi Manula na ndio sababu hayupo kambini nchini Misri.

Kumekua na tetesi kua klabu ya Simba inafikiria kuingia sokoni kufanya usajili wa golikipa mwingine kuelekea msimu mpya, Lakini mpaka sasa hakuna maamuzi yeyote yaliyofikiwa ya kuingia sokoni kisa majeraha ya golikia Ayoub Lakred ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa takribani wiki sita.

Acha ujumbe