Sakata la Kagoma Lipo Kwenye Sura Hii.

YANGA wamewasilisha nyaraka mbili muhimu kwenye shauri linaloendelea la kimkataba kati yao na Mchezaji Yusuph Kagoma pale TFF. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Yanga kabla ya kuongea na Mchezaji waliwasiliana na Fountain Gate juu ya uwezekano wa kumpata Mchezaji huyo ambapo Fountain walitoa ruhusa ya mazungumzo kufanyika ambapo baadae wakasaini rasmi SALES AGREEMENT (Makubaliano ya mauzo) walisaini MACHI 27, 2024.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Kwa upande wa Yanga alisaini CEO ANDRE MTINE na FGA alisaini CEO THABITA ilikuwa siku ya JUMATANO majira ya mchana! Baada ya hapo Yanga wakamalizana na FGA tena zilikuwa contract mbili nyingine ya NICKSON KIBABAGE na zote wakalipwa.

Kilichofuata ni YANGA na Mchezaji YUSUPH KAGOMA ambapo alisafirishwa kutoka Kigoma mpaka Dar Es Salaam na kusaini Mkataba sio mkataba wa awali bali MKATABA mnamo tarehe 28 MACHI, 2024 mbele yake na Shahidi akiwa ni Mwanasheria wake.

IKUMBUKWE, nyaraka zote tajwa hapo juu zimewasilisha mbele ya KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI TFF ndio hizo nyaraka muhimu za kuamua mgogoro huo, hivyo ni kweli FGA walifanya biashara na ni kweli KAGOMA alisaini YANGA.

Kwanini Yusuph Kagoma hataki kucheza Yanga baada ya kusaini? Awali iliripotiwa kuwa hakulipwa fedha zake kwa wakati ila mkataba unasema alipaswa kulipwa JULAI MOSI, 2024 kwa mujibu wa Mkataba hivyo Yanga walikuwa ndani ya makubaliano.

YANGA pia walipewa taarifa kuwa Mchezaji hataki kucheza Yanga kwakuwa haioni nafasi yake, YANGA walikuwa tayari kumruhusu ila WALICHUKIZWA na dharau pamoja na kejeli zilizoanza hivyo walitoa masherti mawili tu, MCHEZAJI AOMBE MSAMAHA mwenyewe ama alipe Fidia ili aondoke.

Mpaka sasa KAMATI YA SHERIA imeiagiza TFF na Bodi waitaarifu Simba isitishe mara moja kumtumia KAGOMA kwakuwa tayari ana pingamizi, YANGA nao wanasema Mchezaji AKIOMBA MSAMAHA wataondoa pingamizi nje na hapo shauri litaendelea kwakuwa wana HAKI hiyo na mikataba ipo wazi.

Ni hayo kutoka KARUME! YANGA wapo tayari kumsamehe Kijana ila anapaswa kuomba radhi hadharani.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe