Laporta Afurahishwa na Flick

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amezungumza juu ya muenendo wa kocha mpya ndani ya klabu hiyo Hans Flick raia wa kimataifa wa Ujerumani ambaye anaonekana kuanza vizuri.

Laporta amezungumza na waandishu wa habari amezungumza namna anafurahishwa na mwenendo wa Flick ndani ya klabu ambapo mpaka sasa kocha huyo amefanikiwa kuanza vizuri ndani ya timu hiyo, Kwani mpaka sasa kocha huyo ameshafanikiwa kushinda michezo yote mitatu ya ligi kuu ya Hispania na kukaa kileleni kwenye msimamo wa La Liga.laporta“Hansi Flick ana nia ya kushinda, tunafuraha kubwa na tunajivunia kikosi chetu.”

“Tunaona La Masia kama msingi wa mradi wetu.”

“Pia tunafurahia sana kazi ya Deco; alifanya kazi bora na ya ajabu pia katika kumleta Hansi Flick hapa.”

Kocha Hans Flick ameonekana kuibadilisha klabu ya Barcelona kwa kipindi cha muda mfupi na kuanza kuonekana klabu inaweza kurejea kwenye ubora wake ambao ilikua nao miaka kadhaa nyuma, Jambo ambalo limemfanya rais wa klabu hiyo Joan Laporta kummwagia sifa nyingi kocha huyo.

Acha ujumbe