Manchester United Wana imani na Ten Hag

Uongozi wa klabu ya Manchester United chini ya mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Omar Berrada wameweka wazi kua wana imani kubwa na kocha wa klabu hiyo mdachi Erik Ten Hag licha kutokua na matokeo mazuri.

Klabu ya Manchester United haijafanikiwa kuanza vizuri msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kupokea vichapo viwili mfululizo kwenye ligi hiyo, Jambo ambalo limeanza kuwapa shaka mashabiki wa klabu ya Manchester United lakini uongozi umeweka wazi kua bado una imani kubwa na kocha huyo.ten hagWakati akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa klabu ya Manchester  United Omar Berrada na kuulizwa kama wana imani na kocha huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi kama uongozi na mkurugenzi huyo kujibu kwa kusema Tunadhani Erik ndiye kocha sahihi kwetu na tunamuunga mkono kikamilifu.

Mpaka sasa kocha Erik Ten Hag ameonekana kupewa ushirikiano mkubwa na uongozi wa klabu hiyo sio tu mkurugenzi wa klabu hiyo, Lakini pia mkurugenzi wa michezo klabuni hapo bwana Dan Ashworth pia amesema anaamini kocha huyo ndio mtu sahihi kwasasa kwenye mradi wao wa miaka kadhaa mbele.

Kocha Ten Hag na kikosi chake walipokea kichapo cha mabao matatu kwa bila wakiwa katika dimba la nyumbani la Old Traffrod hapo wakiwa wametoka kupoteza mchezo dhidi ya Brighton wiki moja nyuma, Hii ikiwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuanza kukosa imani na kocha huyo ambaye ameonekana kupewa ushirikiano mkubwa na uongozi haswa kwenye usajili katika dirisha hili kubwa.

Acha ujumbe