Manchester United Dhidi ya Fulham Kuifungua EPL Leo

Klabu ya Manchester United leo itaufungua msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza 2024/25 wakikipiga dhidi ya klabu ya Fulham mchezo utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.

Manchester United baada ya muda mrefu kupita wanacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza wakianza safari ya kulitafuta taji la hilo baada ya kulikosa kwa takribani miaka kumi, Fulham ndio watakua kipimo cha kwanza cha vijana wa kocha Erik Ten Hag msimu huu.manchester unitedMan United wana maingizo kadhaa mapya kwenye kikosi chao ambayo kwa asilimia kadhaa yanaweza kuanza katika mchezo wa leo wa ufunguzi, Wachezaji hao ni De Ligt pamoja na Mazraoui ambao wamefanya mazoezi na kikosi hicho kwa siku mbili lakini wanaweza kuanza katika mchezo wa leo kutokana na majeraha yanayokiandama kikosi hicho.

Mchezaji kama Noussair Mazraoui anaweza kucheza kama beki wa kushoto kutokana na majeraha ambayo yanamuandama beki Luke Shaw, Huku De Ligt akicheza eneo la kati kutokana na kukosekana kwa beki Leny Yoro majeraha yanaweza kua sababu ya wachezaji hao kuanza katika mchezo wa leo.manchester unitedKikosi cha Manchester United hakikua na msimu mzuri kwenye ligi kuu ya Uingereza licha kubeba taji la FA ambapo walimaliza nafasi nane kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Hivo msimu huu wanaonekana kuhitaji kubadilisha matokeo ya msimu uliomalizika na ndio sababu ya kufanya sajili kadhaa za kuboresha timu hiyo.

Acha ujumbe