Kompany Ahaidi Makubwa Mchezo wa marudino Dhidi ya PSG

Kocha Vincent Kompany amesema timu yake ya Bayern Munich iko tayari kufanya makubwa zaidi katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Paris Saint-Germain, kufuatia mchezo wa kwanza ulioisha kwa kipigo cha mabao 5-4 nchini Ufaransa. Mchezo huo uliweka rekodi ya kuwa na mabao mengi zaidi katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Kompany Ahaidi Makubwa Mchezo wa marudino Dhidi ya PSGBayern walikuwa wa kwanza kupata bao kabla ya kuruhusu kufungwa mabao matano, lakini walipambana na kufanikiwa kupunguza tofauti hiyo kwa kufunga mabao mawili katika kipindi cha pili, wakionesha uwezo mkubwa wa kushambulia licha ya matokeo hayo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kompany alitoa kauli fupi lakini yenye uzito akisema “Zaidi. Hata zaidi,” akimaanisha mashabiki wanapaswa kutarajia burudani kubwa zaidi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nyumbani Allianz Arena mbele ya mashabiki zaidi ya 75,000.“Tunacheza nyumbani, tutakuwa na mashabiki 75,000. Hatutaki kelele tu, tunahitaji nguvu kubwa ya pamoja kutoka kwa mashabiki. Huu si uwanja usiozoea mafanikio kwa timu hii,” alisema Kompany akisisitiza umuhimu wa sapoti ya mashabiki.

Kompany Ahaidi Makubwa Mchezo wa marudino Dhidi ya PSGKatika msimu huu, Bayern tayari wameweka rekodi kadhaa ikiwemo kufunga mabao 113 katika ligi ya Bundesliga, wakivunja rekodi ya muda mrefu ya mabao 101 iliyowekwa msimu wa 1971/72. Aidha, kwa mara ya kwanza, wachezaji watatu wa Bayern ambao ni Harry Kane, Michael Olise na Luis Diaz wamehusika moja kwa moja katika mabao 10 au zaidi kila mmoja kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa.

Kompany Ahaidi Makubwa Mchezo wa marudino Dhidi ya PSGKompany aliongeza kuwa licha ya kuruhusu mabao matano, timu yake bado ina nafasi kubwa ya kufanya maajabu nyumbani “Ukiruhusu mabao matano katika Ligi ya Mabingwa, kwa kawaida unakuwa umetoka, lakini sisi tulifunga mabao manne Paris. Tunaweza kufunga mabao, tumethibitisha hilo na tutafanya hivyo tena nyumbani.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.