Manchester United Bado inawapigia Hesabu De Ligt na Mazraoui

Klabu ya Manchester United inaelezwa bado inawapigia hesabu mabeki wawili wa klabu ya Fc Bayern Munich Noussair Mazraoui na Mathijjs De Ligt kuelekea mwishoni wa dirisha hili.

Mazungumzo yanaendelea baina ya vilabu ya Bayern Munich na Manchester United kwajili ya kukamilisha dili la wachezaji hao wawili ambapo mpaka sasa hawajafikia makubaliano, Mpango wa klabu ya Bayern Munich upo palepale ambao unaelezwa ni kuwauza wachezaji hao katika dirisha hili.manchester unitedVyanzo kutoka ndani ya Man United vinaeleza kua klabu hiyo itahakikisha ndani ya mwezi huu wanakamilisha dili la wachezaji hao kwakua kwasasa wanatafuta njia ya kuweza kumalizana na Bayern Munich, Uzuri ni kua Mashetani wekundu wanajua kua Bavarians hawana mpango na wachezaji hao hivo mwisho watawauza tu.

Wachezaji De Ligt na Mazraoui wanaelezwa wote wanasubiria vilabu hivo kumalizana ili wajiunge na klabu ya Manchester United kwakua wanaelezwa wamepiga chini ofa ya vilabu vingine kwajili ya kujiunga na Manchester United, Hii inaelezwa inatokana na ushawishi mkubwa kutoka kwa kocha wao wa zamani Erik Ten Hag.

Acha ujumbe