Klabu ya Manchester United inaelezwa kuwinda saini ya kiungo wa klabu ya Burnley ambayo imeshuka daraja Sander Bergre raia wa kimataifa wa Norway kuelekea msimu mpya wa 2024/25.
Manchester United mpaka sasa hawana matumaini ya kumpata kiungo Manuel Ugarte wa PSG ambaye walikua wanamfuatilia kwa karibu baada ya kushindwa kufika bei, Lakini pia wachezaji wengine wa eneo hilo wameonekana kua na gharama kubwa hivo wameamua kumtupia macho kiungo Sander Berge.Kiungo Sander Berge amekua na msimu mzuri sana ndani ya klabu ya Burnley chini ya kocha Vicent Kompany licha ya ksuhuka daraja kwa timu hiyo, Lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Norway alikua mchezaji mzuri na ndio klabu ya Man United wamemuona kama kiungo ambaye atawafaa kwasasa sokoni.
Frenkie De Jong bado anahusiswa na klabu ya Manchester United lakini mashetani wekundu wanaelezwa hawana mpango na kiungo huyo kwasasa baada ya kushindwa kukamilisha dili la Ugarte, Nguvu zao zote wamezihamishia kwa kiungo Sander Berge ambaye amekua kwenye kiwango kizuri sana ndani ya klabu ya Burnley.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.