UONGOZI wa Fountain Gate umeweka wazi kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kuelekea Tanzanite Day linalotarajiwa kufika kilele chake rasmi Agosti 9 2024 ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kila kitu kipo kwenye mpangilio wake.
Maandalizi yamepamba moto kwa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara kukamilisha usajili wa wachezaji wapya kwenye timu zote mbili ikiwa ni pamoja na ile ya Wanawake.
Issa Liponda wengi wanapenda kumuita Mbuzi ambaye ni Ofisa Habari wa Fountain Gate amebainisha kuwa maandalizi yapo vizuri kuelekea kilele cha Tanzania Day ambapo wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
“Tupo vizuri kuelekea Tanzanite Day na tunatarajia kuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya mchezo utakachezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa hapo tutambulisha wachezaji wetu na benchi la ufundi na kutakuwa na michezo mbalimbali ya kirafiki kabla ya kuhitimisha tamasha letu.