Solanke Huyoo Spurs

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Fc Bournamouth Dominik Solanke amefanikiwa kujiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs mapema jioni ya leo.

Tottenham wamefanikiwa kutoa kiasi cha paundi milioni 65 kwa klabu ya Bournamouth kwajili ya kupata huduma ya mshambuliaji Solanke, Hivo kwasasa Spurs wamefanikiwa kupata mshambuliaji ambaye amekua kwenye ubora ambao klabu hiyo ilikua inautaka.solankeMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua na msimu bora sana uliomalizika baada ya kufanikiwa kufunga mabao 19, Huku ukiwa ni msimu bora sana kwa mshmbuliaji huyo na kua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha Bournamouth chini ya kocha Andoni Iraola.

Kikosi cha Tottenham Hostpurs chini ya kocha Ange Postecoglou msimu uliomalizika alieleza kua klabu yake inahitaji mabadiliko kwa kiwango kikubwa na moja ya maeneo ambayo alihitaji yafanyiwe mabadiliko ni eneo la ushambuliaji, Hivo kumpata Dominik Solanke ni ishara tosha kua mabosi wa klabu wamefanya ambacho kocha alikihitaji.

Acha ujumbe