Tottenham Yamvizia Solanke

Klabu ya Tottenham inaelezwa kufukuzia saini ya mshambuliaji wa klabu Bournamouth Dominik Solanke raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye anafasnya vizuri kwasasa.

Tottenham wanatafuta mshambuliaji ambaye ataweza kusaidiana na Richarlison raia wa kimataifa wa Brazil ambaye amekua akiandamw ana majeraha ya mara kwa mara, Hivo majogoo hao wa London wamekua wakihitaji mshambuliaji mwingine ambaye atakua na uwezo wa kufunga mabao kwa kiwango kikubwa.tottenhamSolanke alikua moja ya washambuliaji bora msimu uliomalizika akiwa amefanikiwa kufunga magoli (19) akiwa nyuma ya wachezaji wa tatu ambao walimpita mabao, Hii ni moja ya sababu ambazo zimewavutia Spurs kuhitaji saini ya mchezaji huyo ambaye amekua na msimu bora sana wa 2023/24.

Kumpata Dominik Solanke sio jambo ambalo litakua rahisi kwa klabu ya Tottenham kwani Bournamouth nao wanataka kuendelea kusalia nae, Hivo Spurs wanapaswa kukaza msuli kwelikweli ili kupata saini ya mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye amekua kwenye kiwango bora kwasasa.

Acha ujumbe