Greenwood Aanza kwa Kishindo Marseille

Winga wa zamani wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ameanza kwa kishindo ndani ya klabu yake mpya ya Olympique Marseille akisaidia klabu yake kupata ushindi wa mabao matano kwa moja.

Greenwood jana alifanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao matano kwa moja waliopata Olympique Marseille na kutengeneza bao moja, Mchezaji huyo anaonekana ni kama amezaliwa upya chini ya kocha Roberto De Zerbi akitabiriwa kufanya makubwa ndani ya klabu hiyo kutoka nchini Ufaransa.greenwoodWinga huyo ambaye alikipiga klabu ya Getafe msimu uliomalizika kwa mkopo na baada ya kumalizika wakahitaji kumbakiza kwa muda mrefu zaidi, Lakini Getafe hawakua na kiwango cha pesa ambacho Manchester United walikihitaji hivo wakapigwa bao na klabu ya Marseille.

Kocha wa klabu ya Olympique Marseille Roberto De Zerbi amemmwagia sifa Greenwood na kusema ni mchezaji wa daraja la dunia na ana uwezo wa kufanya makubwa sana, Huku akisisitiza watu waachane na yaliyopita waangalie kilichopo na zaidi ni kumpa ushirikiano mchezjai huyo ili aendelee kufanya makubwa zaidi.

Acha ujumbe