Napoli Yamchukua Neres

Klabu ya Napoli inaendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2024/25 baada ya kufanikiwa kunasa saini ya winga wa kimataifa wa Brazil aliyekua anakipiga klabu ya Benfica David Neres.

Napoli wamefikia makubaliano na klabu ya Benfica ya kiasi cha Euro milioni 30 kupata saini ya David Neres ambaye atakwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi cha mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A chini ya kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus Antonio Conte.napoliKocha Antonio Conte anapambana kuhakikisha anairejesha klabu hiyo kwenye ubora ambao ilikua nao misimu miwili nyuma mpaka kufikia kubeba ubingwa wa ligi hiyo, David Neres ni moja ya wachezaji ambao ameonekana kama anaweza kurudisha uhai kwenye klabu hiyo na ndio maana wamemsajili.

Winga David Neres ni moja ya mawinga ambao wanafanya vizuri barani ulaya jambo ambalo liliwavutia klabu ya Napoli kufanya usajili wake kutoka klabu ya Benfica, Winga huyo wa kimataifa wa Brazil kuanzia msimu ujao atawatumikia mabingwa hao ligi kuu ya Italia msimu wa 2022/23.

Acha ujumbe