Swali kubwa leo ni je klabu ya Chelsea itaendelea ilipoishia msimu uliomalizika walipocheza dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza ambapo hawakufungwa katika michezo yote miwili waliyokutana ya ligi kuu ya Uingereza.
Ni wazi klabu ya Chelsea licha ya kutokua na msimu mzuri lakini ni moja ya timu ambazo ziliwapa wakati mgumu sana vijana wa Pep Guardiola msimu uliomalizika, Kwani michezo yote miwili waliyokutana kwenye ligi hiyo ilimalizika kwa sare ya kufungana jambo ambalo linasubiriwa kama litatokea tena leo.Mchezo wa leo utapigwa pale katika dimba la Stamford Bridge ambapo wenyeji ni matajiri hao wa jiji la London wakiwakaribisha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City ambayo ni wazi ndio klabu namba moja kwa ubora kwasasa ndani ya ardhi ya Uingereza.
Klabu ya Chelsea chini ya kocha mpya Enzo Maresca anakwenda kuanza safari yake ya matumaini ya kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora wake ambao imekua nao kwa miaka minne nyuma, Inaweza kua bahati nzuri au mbaya kwake kwani anakwenda kuanza dhidi ya bingwa mtetezi wa ligi hiyo klabu ya Man City.Matajiri hao wa jiji la London wanaelezwa wanaweza kumkosa nahodha wao Reece James katika mchezo wa leo ambaye alipata majeraha siku chache zilizopita, Huku Manchester City nao ikiripotiwa wanaweza kumkosa moja ya mchezaji bora kikosi raia wa kimataifa wa Hispania kiungo Rodri lakini kwa kiwango kikubwa vikosi vyote vimetimia.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.