Chelsea Wamalizana na Neto

Klabu ya Chelsea sasa wamefanikiwa kukamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Ureno Pedro Neto ambaye alikua anakipiga katika klabu ya Wolverhampton Wanderers.

Chelsea wametumia kiasi cha Euro milioni 60 kuhakikisha wanapata saini ya winga huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye hakua anazngumziwa na klabu ya Chelsea, Lakini hatimae umekua mchakato wa muda mfupi na dili limekamilika mapema mchana wa leo.chelseaChelsea wamekua wakifanya usajili mara kwa mara lakini wachezaji wengi ambao wamewasajili sio wenye uzoefu mkubwa wengi wao ni vijana wadogo, Lakini kwa Pedro Neto ni tofauti kwakua ni mchezaji ambaye amekua na uzoefu wa kucheza ligi kuu ya Uingereza kwa zaidi ya msimu mmoja.

Matajiri hao wa London wamefanikiwa kukamilisha usajili huo baada ya kukubaliana maslahi binafsi kwanza na mchezaji huyo pamoja wakala wake Jorge Mendes, Kilichobaki kwa mchezaji huyo ni kufanya vipimo vya afya ndani ya timu hiyo na baadae kusaini mkataba ndani ya viunga vya Stamford Bridge kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe