Simba Yaanza Vizuri NBC 2024/25

Klabu ya Simba imefanikiwa kuanza vizuri msimu mpya wa ligi kuu ya NBC 2024/25 kwa ushindi mnono wa mabao matatu kwa bila mbele ya klabu ya Tabora United kutoka mkoani Tabora.

Simba walionekana kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo wanaitaka mechi na wanataka kupata matokeo jambo ambalo liliwafanya kutangulia kupata goli kupitia kwa beki wake wa kati Che Fondo Malone ambaye alipokea pasi safi ya kiungo Jean Charles Ahoua mnamo dakika ya 14 ya mchezo.simbaWekundu wa Msimbazi waliendelea kumiliki mchezo kwa kiwango kikubwa na kuendelea kufika langoni mwa timu ya Tabora Fc mara kwa mara lakini hawakufanikiwa kupata bao la pili ndani ya kipindi cha kwanza ambapo mchezo ulienda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa goli moja tu.

Kipindi cha pili kilirejea kilianza kwa Wekundu wa Msimbazi kuendelea kumiliki mchezo kwa kiwango kikubwa wakitengeneza nafasi mara kadhaa kuangalia namna ya kuongeza goli, Mnamo dakika ya 69 ya mchezo nahodha Mohamed Hussein alipiga krosi safi ambayo ilimaliziwa vizuri na mshambuliaji Valentino Mashaka na kufanya klabu hiyo kuongeza uongozi.

Klabu ya Simba walijihakikishia alama tatu muhimu mnamo dakika ya 92 ambapo kiungo Awesu Ally Awesu alipiga msumari wa tatu na kuhakikisha mnyama anaondoka na alama zote tatu na magoli matatu, Hivo Wekundu wa Msimbazi ligi wameianza vizuri kinachosubiriwa ni mwendelezo wa michezo yao ya mbeleni.

Acha ujumbe