Manchester United Yamuuza Kinda wake Oyedele

Klabu ya Manchester United imemuuza kiungo wake kinda mwenye kipaji kikubwa kwenda klabu ya Legia Warsaw ya nchini Poland baada ya kukaa klabuni hapo kwa muda mrefu.

Maxi Oyedele mwenye umri wa miaka (20) amekaa ndani ya Manchester United kwa miaka 12 ambapo alijiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka nane, Ambapo hapo katikakati alitolewa kwa mkopo vilabu vingine kadhaa lakini mchezaji huyo amekaa ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu.manchester UnitedKiungo huyo ameona ni wakati sahihi wa yeye kwenda kutafuta changamoto nje ya Man United na hii inatokana na yeye kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye timu ya wakubwa, Hivo kujiunga na Legia Warsaw ya nchini Poland anaweza kuonesha kipaji chake na kurejea tena ndani ya Man United kama watamuhitaji.

Wachezaji kadhaa vijana wametangaza kuondoka ndani ya Manchester United katika dirisha hili la majira ya kiangazi akiwemo na kiungo huyo fundi Maxi Oyedele raia wa kimataifa wa Poland, Hii inatokana na kutokuona kesho yao yenye nuru ndani ya Man United kutokana na kukosa nafasi ya kucheza.

Acha ujumbe