Manuel Ugarte Kucheza Man United kwa Mkopo

Kiungo wa kimataifa wa Uruguay ambaye anafukuziwa kwa karibu na klabu ya Manchester United Manuel Ugarte inaelezwa anakaribia kujiunga na Man United kwa mkopo wa msimu mzima.

Klabu ya PSG na Manchester United ziko mbioni kukubaliana kukamilisha dili la Manuel Ugarte ambaye ameonesha nia ya kujiunga na mashetani wekundu kuelekea msimu ujao, Kwani ameshakubaliana maslahi binafsi na klabu hiyo mwezi mmoja uliomalizika mpaka sasa kinachosubiriwa ni vilabu kukubaliana tu.manuel ugarteTaarifa ambazo zimetoka mchana wa leo ni kua dili hilo lipo kwenye hatua za mwisho na Man United wameshikilia msimamo wao wa kumchukua kiungo huyo kwa mkopo na kukubaliana na kipengele cha kumnunua baada ya mkopo, Hii imetokana na kiwango cha pesa ambacho klabu ya PSG walikua wanakihitaji na Man United hawakua tayari kukilipa kwa kipindi hiki.

Kiungo Manuel Ugarte kujiunga na Manchester United kwasasa ni suala la muda kwakua vilabu vimekaribia kukubaliana kukamilisha dili hilo, Lakini pia mchezaji mwenyewe toka siku ya kwanza amekua akionesha kuvutiwa na kucheza Man United jambo ambalo limerahisisha dili hilo kwa mashetani wekundu.

Acha ujumbe