Manchester United Kinachofuata ni Manuel Ugarte

Klabu ya Manchester United baada ya kukamilisha dili beki wa kimataifa wa Ufaransa Leny Yoro mwenye umri wa miaka (18) sasa wanahamia kwa kiungo wa kimataifa wa Uruguay Manuel Ugarte.

Manchester United wanaelezwa wanataka kukamilisha sajili zao haraka kabla ya msimu wa mwisho ndio maana sajili zao kwasasa hazichukui muda mrefu kwenye mazungumzo, Mfano dili la Yoro limekamilika ndani ya muda mfupi na leo baada ya kukamilika dilo wanahitaji kumaliza dili la Ugarte mapema.manchester unitedMashetani Wekundu wamekua na mazungumzo na klabu ya PSG juu ya kiungo Ugarte na mazungumzo yanaelezwa kua chanya japo makubaliano hayajafikiwa bado, Lakini mipango ya klabu hiyo ni kuhakikisha wanamalizana na kiungo wa kimataifa wa Uruguay siku za hivi karibuni.

Taarifa za ndani kutoka Manchester United zinaeleza klabu hiyo ipo kwenye wakati mzuri wa kupata saini ya kiungo Manuel Ugarte raia wa kimataifa wa Uruguay, Hizi ni zinaweza kua taarifa nzuri kwa mashabiki wa Man Uited kama watafanikiwa kumsajili kiungo huyo kwakua watakua wamefanya maboresho kwenye moja ya maeneo muhimu sana klabuni hapo.

Acha ujumbe