Rabiot Anapatikana Bure Kabisa

Aliyekua kiungo wa klabu ya Juventus Andrien Rabiot ameondoka ndani ya klabu ya Juventus baada ya mkataba wake kumalizika na hii imethibitishwa na miamba hiyo ya soka nchini Italia.

Rabiot anaondoka ndani ya klabu ya Juventus kwa uhamisho huru kabisa hivo klabu ambayo itakayomuhitaji kiungo huyo kwasasa haitakua na ulazima wa kulipa hela ya usajili kwa timu fulani, Lakini badala yake watahitaji kufanya mazungumzo na mchezaji mwenyewe ili kufikia muafaka.RabiotVilabu kadhaa vinatarajiwa kupigana vikumbo kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kutokana na ubora mkubwa ambao anao kiungo huyo, Klabu ya Manchester United imewahi kuhitaji saini ya kiungo huyo na dili liliharibika mwishoni kutokana na kushindwani katika baadhi ya vipengele.

Huu ni ndio unaweza kua wakati wa Manchester United kutamba kwa Rabiot kwani wamekua wakimfukuzia tangu mwaka 2022 na hawakufanikiwa kumpata, Hivo kitendo cha yeye kupatikana kwa uhamisho huru inaweza kua nafuu kwa wao katika wakati huu ambao klabu hiyo inataka kubana matumizi ya pesa.

Acha ujumbe