Wan Bissaka Kutimkia West Ham

Beki wa klabu ya Manchester United Aaron Wan Bissaka anatarajiwa kutimka ndani ya klabu ya Manchester United na kujiunga na klabu ya West Ham United kutoka jijini London.

Klabu ya West Ham inaelezwa wapo mbioni kutuma ofa kwa Manchester United ambao nao wako tayari kumuachia beki huyo, Kwani ni moja ya wachezaji ambao wamepanga kuwaachia klabuni hapo lakini pale tu watakapopata kiwango sahihi cha pesa ambacho wanakitaka.Wan bissakaKlabu ya West Ham wanapaswa kutoa kiasi ambacho kitawashawishi Man United kumuachia beki huyo mwenye asili ya Congo, Wagonga nyundo wa London wanaelezwa wameandaa kiasi cha paundi milioni 15 kwajili ya kupata huduma ya beki Wan Bissaka kuelekea msimu ujao.

Klabu ya Manchester United mpaka sasa wameshakamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao ni mshambuliaji Joshua Zirkzee na beki Leny Yoro, Huku usajili mwingine ambao wanataka kuufanya itategemeana kwa kiwango kikubwa na wachezaji ambao watawauza hivo ni wazi United watahakikisha wanamuuza Wan Bissaka ili waendelee kufukuzia dili la mchezaji mwingine.

Acha ujumbe