Manchester United Yamuwinda Manuel Ugarte

Klabu ya Manchester United ipo mawindoni kwajili ya kumpata kiungo wa kimataifa wa Uruguay Manuel Ugarte anayekipiga ndani ya klabu ya PSG mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa.

Manuel Ugarte amekua anapitia kipindi kigumu akiwa ndani ya klabu ya PSG kwakua tangu ajiunge na klabu hiyo dirisha kubwa lililopita amekua hapati nafasi mara kwa mara jambo ambalo hata yeye limemfanya kufikiria kutimka ndani ya klabu hiyo katika majira haya ya joto.manchester unitedPSG wameweka wazi kua kiungo huyo wa zamani wa Sporting Lisbon ya Ureno atakua sokoni katika majira haya ya joto, Huku Manchester United wao wakielezwa wako tayari kutuma ofa kwajili ya kumpata kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa katika eneo la uzuiaji.

Klabu ya Chelsea waliwahi kumtaka sana kiungo huyu kabla hajajiunga na klabu ya PSG msimu uliomalizika lakini hawakufanikiwa kumpata, Hivo msimu huu wanaweza kujaribu kupeleka ofa kwa mabingwa hao wa Ufaransa ili kupata huduma ya kiungo huyo.manchester unitedMpaka sasa ni klabu ya Manchester United ambayo imeonekana kuhitaji huduma ya Manuel Ugarte hii inaonesha kua kiungo Casemiro anaweza akatimka ndani ya klabu hiyo, Kwani Manuel Ugarte ni kiungo wa ulinzi nafasi ambayo Casemiro anaicheza ndani ya kikosi cha Man United.

Acha ujumbe