Manchester United Yamtaka Van Nistelrooy

Klabu ya Manchester United inamuwinda gwiji wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwasasa ni kocha Ruud Van Nistelrooy kwajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo.

Manchester United wanamtaka mholanzi huyo kwajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la kocha Erik Ten Hag, Klabu hiyo inaelezwa ina mpamgo wa kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo licha ya kumbakiza kocha mkuu wa timu hiyo.manchester unitedVan Nistelrooy alikua anatakiwa na klabu ya Burnley ambayo imeshuka daraja msimu uliomalizika na klabu hiyo ikielezwa ilifika kwenye hatua nzuri dhidi ya Nistelrooy, Lakini Man United kuingilia dili hilo inaweza kubadili kila kitu kwa upande wa Burnley.

Klabu ya Manchester United wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanatengeneza timu bora ambayo itaweza kushindana kuwania mataji na kushinda, Hivo sio wachezaji tu wanaopaswa kua bora lakini ubora unapaswa kuanzia kwenye uongozi na ndio sababu ya kuboresha benchi la ufundi la timu hiyo wakimtaka Ruud Van Nistelrooy.

Acha ujumbe