Manchester United Kufungua Pazia la EPL 2024/25

Klabu ya Manchester United wanatarajiwa kuufungua msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti 16 ambapo watacheza dhidi ya klabu ya Fulham siku ya Ijumaa.

Ni muda mrefu umepita tangu klabu ya Manchester United iufungue msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza lakini mwaka huu shilingi imewaangukia, Ambapo watakua katika dimba lao la nyumbani la Old Trafford wakiwakaribisha klabu ya Fulham kutoka jiji la London.manchester unitedMsimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza kama ilivyo kawaida hua unaanza kutimua vumbi mwezi wa nane na utaratibu umeendelea ambapo ligi hiyo itaanza kutimua vumbi tena mwezi huo Agosti, Huku vilabu ligi ikitarajiwa kua na ushindani mkubwa kutokana na vilabu mbalimbali kutarajiwa kufanya usajili mkubwa wa kuimarisha kikosi chao.

Manchester United ambao wataufungua msimu rasmi dhidi ya Fulham wako wanapambana kufanya sajili zao mapema kwajili ya kukiimarisha kikosi chao mapema ili kuleta ushindani mkubwa katika ligi kuu ya Uingereza pamoja na michuano mingine ambayo watakua wanashiriki.

Acha ujumbe