Manchester United Yalazimishwa Sare Nyumbani

Klabu ya Manchester United wameendelea kudondosha alama katika ligi kuu ya Uingereza baada ya leo kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja na klabu ya Burnley wakiwa nyumbani.

Baada ya kupata matokeo ya ushindi katikati ya wiki dhidi ya Sheffield ilionekana kama Manchester United wangeendelea walipoishia katika mchezo huo, Lakini hali imekua tofauti kwani leo wamekubali kudondosha alama mbili kwenye uwanja wao wa nyumbani.manchester UnitedVijana wa kocha Erik Ten Hag walionekana kutengeneza nafasi nyingi kaika mchezo huo, Lakini matumizi sahihi ya nafasi hizo ndio ilikua tatizo kubwa na hiki kimekua kitendawili ambacho hakijapata wa kukitegua ndani ya kikosi hicho tangu msimu uliomalizika.

Man United walifanikiwa kupata goli la uongozi dakika ya 80 ya mchezo kupitia kwa winga wa kimataifa wa Brazil Antony, Lakini goli hilo halikudumu kwani mnamo dakika ya Buenley walipata goli la kuwazisha kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Zeki Amdouni.manchester UnitedMchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja na Manchester United kuendelea kubaki  nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku matumaini ya kuipata nafasi ya nne yakiendelea kufifia zaidi.

Acha ujumbe