Klabu ya Liverpool imekabwa koo tena leo mbele ya klabu ya Westham United baada ya kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.
Baada ya mchezo wa leo ni wazi Liverpool wameaga mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Kwani mpaka sasa wamecheza michezo 34 wakiwa na alama 75 wakiwa nyuma kwa klabu ya Arsenal kwa alama mbili wakiwa wamewazidi mchezo mmoja.Majogoo wa Anfield leo wamelazimishwa sare na wagonga nyundo wa London wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, Westham ndio walikua wa kwanza kupata goli kupitia kwa Jarrod Bowen dakika ya 23 na mchezo kuenda mapumziko kwa Westham kua mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa vijana wa Jurgen Klopp walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kuweza kusawazisha goli kupitia kwa Andy Robertson dakika ya 48 ya mchezo, Kabla ya golikpa wa Westham Areola kujifunga goli la pili dakika ya 65.Liverpool walipata uongozi wa mabao mawili kwa moja baada ya kutoka nyuma lakini hawakuweza kushikilia uongozi huo mpaka mwisho wa mchezo, Kwani mnamo dakika ya 77 walisawazishia goli na mshambuliaji Antonio na matokeo kua 2-2 na matokeo yalisimama hivo mpaka mwisho wa mchezo.