Juventus Wanamtaka Todibo kwa Mkopo

Klabu ya Juventus inaelezwa inamuhitaji beki wa klabu ya OGC Nice Jean Clair Todibo kwa mkopo ambao una kipengele cha kumnunua kuelekea msimu ujao.

Juventus wamekua wakimfukuzia Todibo kwa takribani wiki tatu sasa ikielezwa kua wameshamalizana na mchezaji huyo kwenye upande wa maslahi binafsi, Huku kilichobakia ni miamba hiyo ya soka kutoka nchini Italia kutuma ofa kwa klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa.juventus

Klabu hiyo kutoka Turin inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa klabu ya West Ham United ya nchini Uingereza ambapo wanaelezwa kutoa dau zuri kwa klabu ya Nice, Hivo inaweza kuwaweka kwenye wakati mgumu miamba hiyo ya soka kutoka nchini Italia kumpata beki huyo.

Beki Todibo ndio anawapa hali ya kujiamini klabu ya Juventus licha hata ya West Ham kutoa dau zuri kwani alishaieleza klabu yake ya Nice kua hataki kwenda West Ham anataka kujiunga na miamba hiyo ya soka ya Italia, Kupitia mchezaji huyo Juventus wanaamini watampata mchezaji huyo kwa mkopo.

Acha ujumbe