Maguire Asisitiza Bado Yupo Sana Man United

Beki wa kati wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Harry Maguire ameweka wazi kua bado yupo sana ndani ya klabu hiyo licha ya tetesi mbalimbali zinazoendelea.

Maguire ameweka wazi kua ameelezwa bado yupo kwenye mipango ya klabu hiyo katika siku za mbeleni hivo anajiona bado klabuni hapo kwa muda zaidi, Hii imekuja baada ya beki huyo kuhusishwa zaidi kutimka klabuni hapo na yeye amefungaka hayo kuonesha bado yupo ndani ya viunga vya Old Trafford.maguireKumekua na tetesi za hapa na pale juu ya kutimka kwa beki huyo wa zamani wa Leicester City ndani ya viunga vya Old Trafford, Lakini beki huyo amevunja ukimya mwenyewe na kusema kua bado yupo ndani ya Man United kuelekea msimu wa 2024/25 na misimu mingine mbele.

Beki Maguire amesema kama klabu ya Manchester United itamueleza kua haina mpango nae siku za mbeleni basi atatafuta sehemu nyingine ya kwenda, Lakini kwasasa yupo ndani ya timu hiyo na ana mkataba wa mwaka mmoja na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe