Beki wa klabu ya Manchester United Harry Maguire inaelezwa amepata majeraha ya misuli ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu na kuelezwa anaweza kurejeas kwenye mchezo wa fainali ya Fa.
Beki Maguire ndio alikua beki wa kati pekee ambae alikua yupo fiti ndani ya kikosi cha Manchester United, Hivo kupata majeraha kwake ni wazi klabu hiyo inakwenda kucheza mchezo wake wa kesho bila beki wa kati aliye fiti.Manchester United imekua ikiandamwa na majearaha sana msimu huu huku kupata majeraha kwa mabeki wa kati wa klabu hiyo kukiwa kumekithiri, Kwani mpaka sasa sio Lindelof, Varane, Lisandro, Johnny Evans, wala Kambwala kijana mdogo walio fiti kucheza ndani ya kikosi hicho.
Joto linaendelea kupanda kwani majeraha haya yanatokea katika kipindi ambacho wanakwenda kukabiliana na klabu ya Arsenal kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza Jumapili Ijayo katika dimba la Old Trafford.Beki Harry Maguire kama ilivyoelezwa anatarajiwa kua fiti kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Fa ambao watacheza dhidi ya klabu ya Man City, Lakini kwa kipindi hichi cha wiki tatu kama mabeki wengine wa klabu hiyo hawatarejea kwenye timu basi klabu hiyo itaendelea kuteseka kwenye eneo hilo.