TABORA UNITED YAINGIA KAMBINI KUMALIZIA MSIMU

Kikosi cha Timu ya Tabora United leo kimeanza maandalizi kwa ajili ya michezo mitatu iliyosalia Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2023/2024.

Mei 22, itamkaribisha Ihefu kutoka mkoani Singida mchezo utakaopigwa saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.tabora unitedTabora United, chini ya Kocha Mkuu Masound Juma Irambona kimeanza kujifua ikiwa ni mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa Mei 09 mwaka huu katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hapa mjini Tabora na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Erick Ukutu.

Tabora United imeanza maandalizi ya michezo hiyo ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mapumziko mafupi yaliyotolewa na Kocha Mkuu Masoud ili kuwaweka sawa wachezaji kimwili na kiakili na hivyo wote wamerudi kwenye uwanja wa mazoezi wakiwa na hari ,morali ya kuwapa furaha mashabikizao kuelekea kwenye michezo hiyo.

Acha ujumbe