Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount atawakosa Arsenal katika mchezo wa jumapili utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.
Kocha wa Man United Eric Ten Hag leo akizungumza na waandishi wa habari ameweka wazi kua kiungo huyo hatakua sehemu ya wachezaji ambao watacheza mchezo wa Jumapili dhidi ya Arsenal kutokana na majeraha mapya ambayo ameyapata.Mount amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara tangu ajiunge na klabu hiyo kwenye dirisha kubwa lililopita jambo ambalo limemfanya kukosa michezo mingi zaidi ndani ya kikosi cha Manchester United msimu huu.
Mbali na kiungo Mason Mount lakini beki Luke Shaw nae hataweza kucheza mchezo huo licha ya kuelezwa kupona majeraha yake, Hii inaonesha kua klabu hiyo itaendelea kumtumia Wan Bissaka kama beki wa kushoto kwenye mchezo dhidi ya Arsenal.Klabu ya Manchester United inaweza kua klabu inayoongoza kwa kukubwa na majeraha msimu huu, Kwani mpaka sasa wamesharipoti kesi za majeraha ya wachezaji hao mara 65 ndani ya msimu huu jambo ambalo linaonekana kuchangia klabu hiyo kutokufanya vyema msimu huu.