Mason Mount Kurejea Baada ya Mapumziko ya Kimataifa

Kiungo wa klabu ya Manchester United Mason Mount ambaye amekua akisumbuliwa na majeraha msimu huu inaelezwa atarejea ndani ya timu hiyo baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.

Mason Mount amekua akisumbuliwa na majeraha ambayo yamemueka nje ya uwanja kwa muda mrefu, Kocha Ten Hag amefunguka leo mbele ya waandishi wa habari kua kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza atarejea baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.MASON MOUNTMchezaji huyo amekua hana wakati mzuri tangu ajiunge na timu hiyo jambo ambalo limemfanya kukosekana katika michezo mingi zaidi ya klabu, Lakini kocha ameweka wazi yuko mbioni kurejea ndani ya kikosi hicho.

Baada ya kocha Ten Hag kuweka wazi kua Mason Mount atarejea ndani ya kikosi hicho baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa, Lakini pia ameweka wazi pia mshambuliaji Hojlund atarejea kwenye mchezo baina ya Liverpool.MASON MOUNTMashabiki wa klabu ya Manchester United wana hamu kubwa ya kumuona Mason Mount anarejea uwanjani, Kwani kiungo huyo alitarajiwa kufanya makubwa ndani ya timu hiyo lakini mpaka sasa matokeo yamekua tofauti sio kama ilivyotarajiwa.

Acha ujumbe