Mason Mount Apata Majeraha Tena

Kiungo wa klabu ya Manchester United Mason Mount imetaarifiwa amepata majeraha tena ikiwa ni mara ya pili tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Chelsea dirisha kubwa lililopita.

Kiungo Mason Mount ameripotiwa kupata majeraha leo na mpaka sasa haijafahamika atakaa nje kwa muda gani, Lakini taarifa kutoka kwa Man United inasubiriwa ili kujua mchezaji huyo atakaa nje kwa muda gani.mason mountManchester United inaandamwa na majeraha sana msimu huu kwani akipona mchezaji mmoja mwingine anapata majeraha, Kwani juzi taarifa za kupona kwa beki Luke Shaw zilitoka leo kiungo huyo anaripotiwa kupata majeraha.

Kiungo huyo ameumizwa na majeraha ambayo ameyapata kwa mara nyingine, Kwani alikua anajituma kwa kiwango kikubwa ili kurejesha ubora wake baada ya kuanza vibaya ndani ya klabu ya Manchester United.mason mountMason Mount atasubiri vipimo vya jopo la madaktari kujua atakaa nje ya uwanja kwa muda gani, Kwani hali imekua sio nzuri kwake ndani ya klabu hiyo mpaka sasa kutokana na kupata majeraha ya mara kwa mara.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.