Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount anatarajiwa kukipiga leo katika mchezo wa kombe la Carabao dhidi ya klabu ya Crystal Palace.
Mason Mount ambaye amekua nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu sasa kutokana na majeraha ana asilimia kubwa za kucheza mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Crystal Palace na anatarajiwa kuanza mchezo huo.Kiungo huyo bado hajafanikiwa kuonesha cheche ndani ya klabu hiyo tangu atue klabuni hapo dirisha kubwa lililopita, Lakini mchezaji huyo anatazamiwa kufanya makubwa ndani ya klabu hiyo kutokana na ubora ambao alikua anauonesha ndani ya Chelsea.
Manchester United haijafanikiwa kuanza vizuri msimu ndani ya ligi kuu ya Uingereza na ligi ya mabingwa ulaya, Lakini sababu mojawapo ya sababu ya kutokufanya vizuri kwa klabu hiyo ni majeraha ambayo yanawaandama wachezaji wake akiwemo na kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza.Kiungo Mason Mount anatazamiwa kama mchezaji muhimu wa klabu hiyo kwa siku zijazo, Kwnai kusajiliwa kama usajili wa kwanza kabisa klabuni hapo dirisha lililopita ilitoa taswira kua ni mchezaji wa aina gani Man United wamemsajili na leo rasmi anarejea kwenye kikosi cha timu hiyo.