Mason Mount Atambulishwa Rasmi Man United

Mason Mount aliyekua mchezaji wa klabu ya Chelsea rasmi sasa ametambulishwa kama mchezaji wa klabu ya Manchester United kuelekea msimu ujao.

Mason Mount amekamilisha dili la kujiunga na klabu yake mpya ya Manchester United kiasi cha paundi milioni 55 na nyongeza ya paundi milioni tano ambayo itaongezwa hapo baadae kwa vipengele ambavyo klabu hizo wamekubaliana.mason mountManchester United wamefanikiwa kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ikiwa wanaonesha njaa yao ya kutaka kuimarisha eneo la katikati ya uwanja ambalo limekua likikosa watu mbadala ambapo wachezaji wengine wanakua wanakosekana.

Mason Mount amefanikiwa kua usajili wa kwanza wa klabu ya Manchester United katika dirisha hili kubwa na mashabiki wa klabu hiyo wameonekana kupokea kwa shangwe ujio wa kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ndani ya viunga vya klabu hiyo.mason mountMashabiki wa Manchester United wameonekana kugawanyika kwa Mason Mount kwenye suala la jezi ambapo kiungo huyo amekabidhiwa jezi namba saba jambo ambalo mashabiki wengine wakiona ni sawa na wengine wakiona sio sahihi.

Acha ujumbe