Simba Yarudi kwa Elia Mpanzu

Klabu ya Simba imerejea kwenye mbio za kumuwania winga wa klabu ya As Vita kutoka nchini Congo Elia Mpanzu ambaye amekua akifukuziwa kwa muda mrefu na klabu hiyo.

Simba imefanikiwa kutuma ofa mara kadhaa kwa klabu ya As Vita wakihitaji kupata saini ya winga Elia Mpanzu lakini ofa hizo zilipigwa chini kwakua hazikukidhi matakwa ya klabu hiyo kuyoka nchini Congo, Lakini Wekundu hao wa Msimbazi wanaelezwa hawajakata tamaa kwakua wanamuhitaji kwelikweli mchezaji huyo.simbaElia Mpanzu yupo kwenye orodha ya juu ya wachezaji ambao wamekua wanahitajika na klabu hiyo kuelekea msimu wa 2024/25 lakini hawakufanikiwa kutokana na ofa yao kutofika ofa ambayo wanaitaka As Vita, Lakini inaelezwa wametuma ofa ya mwisho ambayo ni dola za kimarekani laki mbili ambayo ni sawa kiasi cha shilingi milioni mia tano na zaidi za Kitanzania.

Klabu ya Simba inaelezwa imeamua kurudi kwenye mbio za kumuwania Elia Mpanzu licha ya kuonekana kua ngumu hapo mwanzo, Hii inaelezwa imetokana na sintofahamu ya winga wa klabu hiyo Kibu Denis ambaye ameibua utata klabuni hapo siku za hivi karibuni kutokana na kushindwa kufika kambini kujumuika na wenzake na kusemakana amepata timu nyingine nchini Norway.

Acha ujumbe