West Ham Wanamtaka Duran

Klabu ya West Ham ipo kwenye mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa Jhon Duran kwajili kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu wa 2024/25.

West Ham imepanga kuboresha ofa yao ambayo waliituma kwa klabu ya Aston Villa ambapo ilipigwa chini hapo awali kudhihirisha wagonga nyundo hao wa London wako makini kukamilisha saini hiyo, Wametuma ofa nyingine ambapo inaelezwa kiwango kimeongezeka tofauti na ilivyokua hapo awali.west hamWagonga nyundo hao wa London wanaelezwa wanataka kuhakikisha klabu yao inarejea kwenye ubora mkubwa ambapo msimu uliomalizika haukufanikiwa kua mzuri kwa upande wa klabu hiyo, Hivo sajili wanazozifanya kwasasa ni kuhakikisha wanairejesha timu hiyo kwenye ubora mkubwa.

Mbali na mshambuliaji Jhon Duran klabu ya West Ham inaelezwa kwasasa wapo mbioni kukamilisha dili la beki wa kulia wa klabu ya Bayern Munich raia wa kimataifa wa Morocco Noussair Mazraoui, Hii inaonesha kwa kiwango gani klabu hiyo imepania kuhakikisha klabu hiyo inarejea kwenye ubora wake chini ya kocha mpya Julien Lopetegui.

Acha ujumbe