Mudathir Yahya Anatoa Majibu Magumu Yanga

KWENYE mechi ngumu ambazo wapinzani wa Yanga walikuwa wakicheza kwa kujilinda zaidi, kiungo Mudathir Yahya alikuwa ni mkali wa kutibua mipango hiyo na kuipa timu hiyo pointi tatu mazima Uwanja wa Azam Complex. Jisajili na Meridianbet upate bonasi kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

 

Mudathir Yahya

Ikumbukwe kwamba Yanga ilipata sare yake ya kwanza msimu wa 2023/23 Februari 2 ubao wa Uwanja wa Kaitaba uliposoma Kagera Sugar 0-0 Yanga ambapo wapinzani wao walitumia mbinu ya kujilinda zaidi.

Ngoma ilikuwa nzito Februari 5 baada ya dakika 85 za kucheza bila kufungwa, Dodoma Jiji walishuhudia bao la jioni likifungwa na Mudathir dakika ya 86 akitumia pasi ya Nickson Kibabage. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Ipo wazi kwamba wakali wote hao wawili walianzia benchi, Mudathir Yahya aliingia dakika ya 61 akichukua nafasi ya Jonas Mkude na Kibabage aliingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya Joyce Lomalisa.

Mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na Mudathir Yahya kutibua mipango kwa bao la usiku ilikuwa dhidi ya Namungo, ilikuwa ni Septemba 20 2023 alipofunga bao dakika ya 87.
Bao hilo alilofunga kiungo huyo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo ilikuwa ni zamani za Cedrick Kaze ndani ya Namungo FC. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.