Feisal Salum, Mudathir Waadhibiwa na Bodi ya Ligi

Viungo wawili Feisal Salum na Mudathir Yahaya wamekumbana na adhabu kutoka kwenye bodi ya ligi kuu ya NBC baada ya kutokupeana mikono na waamuzi na wachezaji wenzao katika mchezo uliokutanisha timu zao.

Feisal Salum na Mudathir Yahaya hawakupeana mikono katika mchezo namba 45 ulivikutanisha vilabu vya Azam Fc na Yanga katika mchezo uliopigwa tarehe 22 mwezi wa kumi katika dimba la Benjamin Mkapa.feisal salumWachezaji hao wamepigwa faini ya shilingi milioni mbili za kitanzania kila mmoja ambapo adhabu hii haijajumuisha kufungiwa michezo na wachezaji hao wataendelea kuvitumikia vilabu vyao sharti ni kulipa kiasi cha milioni mbili kila mmoja.

Tukio hilo lilitokea wakati zoezi la wachezaji kupeana mikono na waamuzi na wenyewe kwa wenyewe, Wachezaji hao wawili walisimama katika mistari ya kuingilia uwanjani na kusubiri mpaka zoezi hilo likakamilika ndio wakaingia.feisal salumKitendo kinatokea mara kwa mara hasa timu kubwa zinapokutana na mbali na Feisal Salum na Mudathir Yahaya, Lakini pia Clatous Chama na Aziz Ki walishakumbana na adhabu baada ya kufanya kitendo kama hicho kukwepa kupeana mikono na waamuzi na wachezaji wenzao.

Acha ujumbe