Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum bado ni mchezaji wa Yanga, kwa mujibu wa mkataba.

 

Feisal Salum bado ni Mali Ya Yanga TFF Yaamua

Uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa Jumatatu, Januari 9 2023.

Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati hiyo ikipinga hatua ya mchezaji wao kuvunja mkataba kati yao bila kuwashirikisha.

Feisal Salum bado ni Mali Ya Yanga TFF Yaamua

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo jana ambapo apnde zote mbili Yanga na kiungo huo ziliwakilishwa na wanasheria wao.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa