Hummels Anukia Bologna

Aliyekua beki kisiki wa klabu ya Borussia Dortmund Matts Hummels raia wa kimataifa wa Ujerumani inasemekana anawindwa kwa karibu na klabu ya Bologna ya nchini Italia.

Bologna wanaelezwa kumshawishibeki Hummels ajiunge na timu hiyo baada ya kumtumia mapngo kazi na mikakati ya klabu hiyo katika siku za mbeleni, Hivo klabu hiyo ambayo imefuzu ligi ya mabingwa ulaya inasubiri jibu la beki huyo kama atasema ndio kupitia mpango kazi waliomtumia.hummelsInaelezwa klabu hiyo imejiandaa kumfanyia vipimo vya afya beki Hummels siku mbili zilizopita lakini wanasubiri beki huyo afanye maamuzi ya kujiunga na klabu hiyo, Beki huyo alitangaza kuondoka ndani ya Dortmund punde tu baada ya kumalizika kwa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika.

Kama beki Hummels atafurahishwa na mipango ya klabu ya Bologna ataweza kujiunga na klabu hiyo kueleka msimu wa 2024/25, Ni wazi klabu ya Bologna watakua wamepata mchezaji mzuri na wa viwango kwakua beki huyo ana uzoefu mkubwa akivitumikia vilabu vya Borussia Dortmund pamoja na Bayern Munich.

Acha ujumbe