Hummels Aondoka Dortmund

Beki wa kimataifa wa Ujerumani ambaye alikua anakipiga ndani ya klabu ya Borussia Dortmund Matts Hummels ametangaza kuondoka klabuni hapo baada ya kudumu klabuni hapo kwa miaka isiyopungua 10.

Matts Hummels ameandika ujumbe kuwashukuru mashabiki wa BVB kwa kipindi chote ambacho ameitumikia klabu hiyo na ushirikiano ambao wamekua wakimpa, Beki huyo anaondoka ndani ya klabu hiyo kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine kwa uhamisho huru.hummels“Wapenzi mashabiki, muda wangu katika rangi nyeusi na manjano unakaribia mwisho baada ya zaidi ya miaka 13. Imekuwa heshima kubwa na furaha kwangu kuichezea BVB kwa muda mrefu na kuwa sehemu ya safari tangu nafasi ya 13 Januari 2008.”

“Makundi mengi ya makocha bora na wachezaji wazuri nimekuwa na heshima ya kukutana nao hapa. Ninawapa dua kuwa mje kukutana tena kwenye Borsigplatz haraka iwezekanavyo kusherehekea.”

“Nitawakumbuka sana.”hummels

Beki huyo amekua mhimili mkubwa sana klabuni hapo haswa katika safari ya klabu hiyo kucheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika, Huku beki huyo akifanikiwa kua nyota wa michezo yote miwili hatua ya nusu fainali dhidi ya klabu ya PSG japokua hakufanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kupoteza mbele ya Real Madrid.

Beki Matts Hummels anaweza kujihesabu kama moja ya mabeki wenye bahati mbaya na taji la ulaya kwani amepoteza fainali mbili za ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich mwaka 2013, na mbele ya Real Madrid mwaka 2024, Lakini pia baada ya kujiunga na Bayern Munich hakufanikiwa kutwaa taji hilo ila aliporejea Dortmund mwaka 2019 mwaka 2020 Bayern Munich walitwaa taji hilo, Zaidi beki huyo atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka ndani ya klabu ya Borussia Dortmund.

 

Acha ujumbe