Branthwaite Aingia Kwenye Rada za Man United

Beki wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya Uingereza Jarrad Branthwaite ameingia kwenye orodha fupi ya wachezaji wanaotakiwa na klabu ya Manchester United kuelekea msimu ujao wa mwaka 2024/25.

Branthwaite ni moja ya mabeki watatu wanaofukuziwa kwa karibu na klabu ya Man United kwajili ya kuboresha klabu yao kwenye eneo la ulinzi msimu ujao, Lakini dau ambalo limetajwa na klabu ya Everton ndio linaonekana linaweza kua kikwazo kwa Man United.branthwaite

Klabu ya Everton inaelezwa kuhita kiasi ya €65 mpaka €70 milioni dau ambalo inaelezwa wanaona wanaweza kupata mchezaji mwingine kama Jean Clair Todibo ambaye wamekua wakimfuatilia toka dirisha kubwa lililopita huku ada yake ya uhamisho ikiwa bei nafuu kuliko beki huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Taarifa zinaeleza beki huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka (21) anataka kujiunga na klabu ya Manchester United, Lakini dau ambalo limetajwa na klabu ya Everton linaweza kua kikwazo kwa yeye kukamilisha usajili huo ambao kama mchezaji anautaka.branthwaiteKlabu ya Manchester United wanaelezwa wataendelea kupambana kuhakikisha wanampata Branthwaite ambaye wanamuwinda kwa karibu zaidi, Lakini wakishindwa kumpata beki huyo bado wana mchaguo mengi ambapo anatajwa beki Jean Clair Todibo anayekipiga klabu ya OGC Nice na Leny Yoro anayekipiga klabu ya Lille.

Acha ujumbe