De Zerbi Akaribia Kutua Marseille

Aliyekua kocha wa klabu ya Brighton Hove and Albion Roberto De Zerbi raia wa kimataifa wa Italia anakaribia kutua kwenye klabu ya Olympique Marseille inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

De Zerbi inaelezwa mpaka sasa amefikia kwenye hatua nzuri na mabosi wa klabu ya Marseille ili aweze kusaini klabuni hapo, Kocha huyo ikumbukwe aliachana na klabu ya Brighton punde tu baada ya msimu kumalizika kwa makubaliano ya pande zote mbili.de zerbi

Taarifa zinaeleza raia huyo wa kimatiafa wa Italia atasaini mkataba wa miaka mitatu ndani ya klabu ya Olympique Marseille, Lakini kocha huyo ikumbukwe aliondoka ndani ya Brighton akiwa na mkataba hivo klabu ambayo itamuhitaji itatakiwa kulipa kiasi cha €6 milioni hivo klabu ya Marseille ndio inafanyia kazi jambo hilo kwasasa.

Kocha huyo ambaye amedumu kwenye klabu ya Brighton kwa takribani miaka miwili akifanikiwa kuonesha soka safi jambo ambalo liliwavutia wengi, Lakini kocha huyo aliamua kutimka klabuni hapo baada ya kukubaliana na mabosi wa klabu hiyo kua anahitaji kupata changamoto sehemu nyingine.de zerbiKocha De Zerbi alikua anahusishwa pia kwa karibu na klabu ya Manchester United baada ya tetesi kuzagaa kua kuna uwezekano wa kocha Erik Ten Hag akatimuliwa klabuni hapo, Lakini inaonekana wazi kua dili hili halitawezekana baada ya Man United kutangaza kumbakiza Erik Ten Hag na kocha huyo wa zamani wa Shakhtar Donetsk sasa ataelekea klabu ya Olympique Marseille.

 

 

Acha ujumbe